ZFA watuma ombi TFF

Chama cha mpira wa miguu Zanzibar kimetuma ombi la kutaka kushirikishwa kwenye mashindano ya taifa ya soka la wanawake. Kwa habari zaidi .....Bonyeza Hapa

Simba wakubali Mapinduzi ya Zanzibar

Klabu ya soka ya Simba imethibitisha kushiriki mashindano ya miaka 51 ya kombe la Mapinduzi ambayo huanza mapema mwezi Januari ya kila mwaka. Kwa habari zaidi......Bonyeza Hapa.

ZFA wafungua dirisha dogo

Wakati ligi kuu ya soka Zanzibar ikienda mapumziko baada ya vilabu vyote kumi na mbili kucheza michezo kumi na moja. Kwa habari zaidi......Bonyeza Hapa

Viongozi wakuu wa mchezo wa mpira wa miguu wa ufukweni maarufu kama Beach Soccer kutoka Zanzibar na Uganda wakitia saini makubaliano yaliyofikiwa na pande hizo mbili juu ya kuendeleza mzhezo huo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

  • Picha ya viongozi wa Grand Malt, ZFA na Waandishi
  • Mkurugenzi wa grand malt akizungumza na viongozi
  • Jeshi la polisi likiwa kazini uwanja wa Amaan
  • Rais wa ZFA Ravia Idarous Faina
  • Mshindi wa mbio za kilimita 10 za KMKM Filipo Jacob.
  • Mkimbiaji wa Kike kutoka KMKM Aldina Edward.
  • Waandishi wakiandaa taarifa za michezo.

Ratiba ya Beach Soccer

Mashindano ya mpira wa miguu wa ufukweni maarufu kama Beach yanaelekea ukingoni Ijumaa tarehe 19/12 Lavista Vs Clove Lodge, B/Sailor Vs ZABECO. Jumamosi 20/12 AZAM Vs N/Generation, Serena Vs ZMCL na Jumapili 21/12 Kilupi Vs Green River. Mechi zote zitachezwa fukwe za Bamboo Bububu kuanzia saa 10:00 za jioni.

Uchaguzi ZFA taifa

Chama cha soka Zanzibar ZFA kinatrajia kufanya uchaguzi wake mkuu Disemba 31 kisiwani Pemba. Hatua hiyo inakuja kufuatia chama hicho kumteuwa Kibabu Haji Hassan kuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi huo akisaidiwa na katibu wake Affan Othman Juma na tayari kamati hiyo imeshatangaza utaratibu wa kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho.